ANAYEKULA

1.    Anayekula mwili wako, na anywaye danu yako,
Anaishi ndani yako, ye hatakufa milele.

Yezu wangu nakuomba, nishibishe na mwilio,
Nayo damu yako ninywe, japo sistahili mimi.

2.    Ndani yangu mwokozi yumo, kwa mwili na damu yake,
Ni rafiki yangu kweli, name sitamwacha kamwe.

3.    Alikuja kutuokoa, tuliokuwa dhambini,
Kwa kifo chake msalabani, naye katupa uzima.

4.    Yezu wangu unibariki, nifundishe njia zako,
Nipe moyo wa shukrani, nitembee nawe leo.

Comments

0 Comments

Login

Welcome! Login in to your account

Remember me Lost your password?

Lost Password