HII NI EKARISTI

1.    Hii ni Ekaristi aliyotuachia
Bwana Yezu Kristu (Kristu), Mkombozi wa dunia.

(Imbeni) Imbeni kwa furaha
(Sifuni) Sifuni ekaristi,
Alimo Yezu Kristu (Kristu),
Alimo ni Mzima.

2.    Yesu katuonea, wema pia huruma,
Alitupenda sana, akatupa uzima.

3.    Jioni alhamisi alichukua mkate,
Kaigeuza mwili, kuleni mkaokoke.

4.    Pia alichukua, kikombe cha divai,
Kaigeuza damu, kunyweni mkaokoke.

5.    Walipo kwishakula, kawaosha miguu,
Nimewapa mfano, fanyeni nanyi pia.

6.    Yezu mwili na damu, chakula cha uzima,
Tujaliwe kupata, uzima wa milele.

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *