1. Nainua moyo wangu, kwako wewe ee Baba;
Unikinge na uovu, tumaini wewe tu.
2. Ni julishe njia zako, ni fundishe ukweli;
Hekimayo niongonze, tumaini wewe tu.
3. Ewe Baba, ukumbuke wema wako milele;
Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu.
4. Nitazame kwa huruma, ewe mungu amini;
Nitubishe, mwante dhambi, tumaini wewe tu.
5. Shida zangu angalia, nikoe dhikini,
Nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu.
6. Nzia zaku zote, Bwana nifadhili,
Niongonze, motto wako, tumaini wewe tu.