HODI BWANA Composed by D. Kalolela

 

Sop: Hodi hodi hodi hodi bwana nifungulie milango nipokee bwana mimi mwano naja kwako leo. Naja kwako bwana kwa magoti na kwa unyenyekevu mkubwa. Hodi bwana nifungulie milango.

 

Alto: Hodi hodi hodi hodi bwana nifungulie milango. Nionye she njia bwana nije kwenye utukufu wako bwana wangu hodi nifungulie milango.

 

Tenor: Hodi hodi hodi hodi nifungulie milango. Hodi bwana hodi nifungulie milango.

Bass: Hodi hodi hodi hodi bwana nifungulie milango.

 

Hodi hodi hodi hodi hodi naja bwana mbele yako kwa unyenyekevu mkubwa ni chague mimi ewe mungu wangu ili ni wa change kondoo zako x2

 

  1. Ee mungu baba mwenyezi wewe wajua yote yaliyomo ndani ya moyo wangu. Wewe bwana wa yajua makossa yangu nisamehe bwana kwani ninkupenda.

 

  1. Nisafishe bwana wangu uovu wangu ili nitakate niwe kama theluji,

Nisimame mbele yako nikiwa safi kwa nuru yako bwana na mimi ning’ae

 

  1. Mbele yake mama yetu Mama Maria najilaza mbele yako kifudifudi

Mbele ya viumbe vyote vya duniani najilaza mbele yako kifudifudi

 

  1. Chini ya jua chini ya mwezi na nyota najilaza mimi bwana unibariki,

Mbele ya hekalu lako ee bwana naja kwaupole kama ndama mkiwa

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *