UTUKUFU KWA MUNGU

Utukufu kwa Mungu mbiguni, na amani duniani, kwa watu wenye mapenzi meema.

1. Utukufu kwa Mungu, heshima kwake Baba, tunakuabudu, twakutukuza ee Baba.

2. Shukrani kwake Mungu, ni Mfalme wa mbiguni, Mwana wa pekee, Mwana wa Mungu Baba.

3. Mwenye kuziondoa, ondoa dhambi zetu,
Ewe ‘tuhurumie, Mwana kondoo wa Mungu.

4. Ewe unayeketi, kuume kwake Baba,
Wewe ndiye uliye, Pekee Mtakatifu.

5. Ewe uliye Bwana, uliye Bwana Mkuu,
Mkombozi wa dunia, pekee yako Kristu.

4. Kwa utawala wako, na Roho Mtakatifu,
Pamoja na Mungu Baba, ‘tukufu ni wako milele.

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *