UTUKUFU KWA MUNGU JUU

Viongozi Wote
‘Tukufu! “Tukufu kwa Mungu juu.
Amani! Na amani duniani
Kwa watu wenye
mapenzi Wenye mapenzi mema. (2)
A — ma — ni !

Sifa! Sisi tunakusifu.
Heshima! Sisi tunakuheshimu.
Tunakuabudu Sisi tunakuabudu. (2)
He – shi – ma!

“Tukufu! Sisi tunakutukuza
Shukrani! Sisi tunakushukuru.
Kwa ‘jili ya utukufu Utukufu wako mkuu. (2)
Shu – kra – ni!

Ee Mungu! Ee Bwana Mungu.
Ee Baba! Mfalme wa mbiguni
Ee Mungu Baba Mungu Baba Mwenyezi.
(2)
Ee – Ba – ba!

Ee Bwana! Ee Bwana Yesu Kristu
Ee Mwana! Kristu Mwana wa pekee
Mwana wa Baba Mwanakondoo wa
Mungu (2)
Ee – Mwa – na!

Mwokozi! Mwenye kuondoa
dhambi
Huruma! Dhambi za dunia
Utuhurumie Pokea ombi letu. (2)
Hu – ru – ma!

Ee Yesu! Kwani ndiwe Mtakatifu
Ee Kristu! Kwani ndiwe Bwana
Ee Yesu Ktistu Ndiwe peke yako Mkuu.
(2)
Ee – Kri – stu!

Umoja! Pamoja na Roho
Mtakatifu
Milele! Katika utukufu
‘Tukufu wa Mungu
Baba Kristu anaishi. (2)
Mi – le – le!

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *