MUNGU BABA POKEA

1. Mungu Baba, pokea sadaka yetu leo,
Twakutoleayo kwa jina la Mwanao;
Kwa Abel na Ibrahinu ilikupendeza,
Yetu Baba ipendeze, upokee tu.

Upokee……………………..Sadaka yetu.
Ndilo fumbo………………la kukupendeza.
La Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu

2. Njoni wote tutoe sadaka yetu leo
Kwa sifa na utukufu wake mwenyezi
Mkate huu na divai view mwili wake,
Kwa heshima kuu sadaka tumutolee.

3. Ee mwenyezi ‘tupokee tuwe mali yako,
Twakusihi kwa shukrani kuu ‘tupokee.
Tunakutolea nguvu, kazi na mavuno,
Kwa huruma yako dhambi ‘tuondolee.

4. Kama mwanzo Mungu Baba nasi asifiwe
Na Mwanaye ndiye aliyetukomboa;
Roho Mtakatifu ndiye wetu mfariji,
‘tata Mtakatifu, Mungu mmoja twakiri.

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *