POKEA VIPAJI

Twakutolea mkate huo
Twakutolea divai hiyo
//Ni kazi ya wanadamu x2

Ee Baba pokea, zawadi tunaleta (x2)
//Pokea Baba hizo zawadi,
Tunaleta kwa Baba Muumba wetu x 2

Twakutolea mazao yetu
Twakutolea na fedha zetu
//Ni kazi ya wanadamu x2

Ee Baba pokea, zawadi tunaleta (x2)
//Pokea Baba hizo zawadi,
Tunaleta kwa Baba Muumba wetu x 2

Twakutolea pokea Baba,
Zikupendeze vipaji vyetu,
//Twavirudisha kwako Baba x2

Ee Baba pokea, zawadi tunaleta (x2)
//Pokea Baba hizo zawadi,
Tunaleta kwa Baba Muumba wetu x 2

Twakutolea na nyoyo zetu,
Twakutolea matendo yetu,
//Yatufae milele yote x2

Ee Baba pokea, zawadi tunaleta (x2)
//Pokea Baba hizo zawadi,
Tunaleta kwa Baba Muumba wetu x 2

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *