TOA NDUGU

Toa ndugu, toa ndugu (2)
Ulicho nacho wewe, bwana anakuona
Mpaka moyoni wako.

1.    Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka,
Kila mtu anze kujifikiria.

2.    Wiki nzima bwana mungu alikulinda vema,
Sasa nawe ndugu yangu ujifikirie.

3.    Kumbuka jinsi Yesu alivyojitolea,
Pale msalabani kwa ajili yetu.

4.    Tolea moyo wako, pia matendo yako,
Naye bwana mungu akubarikie.

5.    Baraka zake mungu, za Baba na za Mwana,
Za Roho mtakatifu zikae nanyi nyote.

Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *