Sasa Ndio Wakati!

Lyrics

1

Sasa ndio wakati, wa kutoa sadaka,
Kila mtu aanze, kujifikiria.

Chorus

Toa ndugu, toa ndugu (2)
Ulicho nacho wewe,
Bwana anakuona, mpaka moyoni mwako.

2

Wiki nzima Bwana Mungu, alikulinda vema,
Sasa nawe ndugu yangu ujifikirie.

3

Kumbuka jinsi Yesu, alivyojitolea
Pale msalabani, kwa ajili yetu

4

Naye Bwana Mungu, akubarikie.
Tolea moyo wako, pia matendo yako,

5

Baraka zake Mungu, za Baba na za Mwana,
Za Roho Mtakatifu, zikae nanyi nyote

Spotted a wrong word or a missing verse? Make corrections